width: 100px; height: 100px; float: right; margin: 15px 25px; background: url(../images/tzflag.gif) no-repeat center center;
 • CCM Blog

  Uimara wa CCM unatokana pia na kuwa na Viongozi Makini Waadilifu

 • CCM Blog

  Uimara wa CCM unatokana pia na kuwa na Viongozi Makini Waadilifu

 • CCM Blog

  Viongozi wa CCM ni HAPA KAZI TU

 • CCM Blog

  Viongozi wa CCM ni viongozi wanajali shida za Watanzania hasa masikini

 • CCM Blog

  Viongozi wa CCM wenye utayari wa kuijenga Tanzania ya Uchumi wa Viwanda

Wednesday, July 19, 2017

TAMKO LA KAMATI YA UTEKELEZAJI YA BARAZA KUU LA UWT KILICHOFANYIKA TAREHE 18/07/2017

Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la UWT imefanya kikao chake cha Kikatiba tarehe 18/07/2017, ambapo pamoja na mambo mengine ilijadili agenda mbalimbali za msingi kuhusu uchaguzi ndani ya Jumuiya. Pia wamejadili juu ya hali ya amani na usalama, uchumi na maendeleo ya Jamii ambapo Kamati imeipongeza Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa mafanikio makubwa ya bajeti ya mwaka 2016/2017, na pia mipango mikubwa ya maendeleo iliyoainishwa kwenye bajeti ya 2017/2018.

KUHUSU UCHAGUZI WA UWT;
Uchaguzi kwa ngazi ya Matawi umefanyika kwa asilimia 95, ngazi ya Kata vikao vya uchujaji vinaendelea na kwa ngazi ya Wilaya, Mkoa na Taifa uchaguzi unaendelea, tarehe 02 – 10/07/2017 wanachama walijitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi, kujitokeza kwao kwa wingi kumethibitisha imani yao kubwa kwa Jumuiya na Chama Cha Mapinduzi. Kwa nafasi ya Mwenyekiti wa UWT waliochukua fomu za kuomba kuteuliwa kugombea ni wanachama 34, nafasi ya Makamu Mwenyekiti wanachama walijotokeza ni 14, wajumbe wa NEC bara 33 Baraza Kuu ni 73 wakilishi Vijana 15na Wazazi 15 Kwa upande wa Zanzibar wajumbe wa NEC 13 wajumbe wa Baraza Kuu ni 40. Jumla ya wanachama waliojitokeza kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa kugombea ngazi ya Wilaya, Mkoa na Taifa jumla yao ni 7,643

Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la UWT imewapongeza wanachama wote waliojitokeza kuchukua fomu za kugombea. Pia, inatoa wito kwa wanachama wote kuendelea kuzingatia Kanuni za Uchaguzi na Maadili kwa kutotangaza nia, kutounda makundi na safu za kampeni pamoja na kujizuia kutoa na kupokea rushwa. UWT inasisitiza kuwa, RUSHWA ni adui wa HAKI. Tutakuwa Jumuiya ya mfano, kwani hatutamvumilia yeyote atakayejihusisha na vitendo vya rushwa.
  
UTEKELEZAJI WA ILANI YA UCHAGUZI;
Kwa namna ya kipekee UWT inaipongeza Serikali kwa utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM wenye mafanikio makubwa wa bajeti ya mwaka 2016/2017 ambapo kwa mara ya kwanza kwenye historia ya nchi yetu makusanyo ya ndani yamefikia takribani Shs. trilion 14.4, makusanyo hayo yakienda sambamba na ukuaji wa uchumi kwa asilimia 7.0% na kupungua kwa mfumuko wa bei kutoka 6.5% hadi kufikia 5.4%.

UWT itanatambua heshima kubwa ambayo nchi yetu imeipata kutoka kwa mataifa ya Afrika na kote duniani kwa kazi kubwa wanayoifanya Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli na Mhe. Rais Dkt. Ali Mohamed Shein ya kurudisha nidhamu ya matumizi Serikali na mapambano yao dhidi ya rushwa.

Kwa msisitizo mkubwa Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la UWT imepongeza ununuzi wa ndege mpya, uamuzi wa kutoa elimu bure na mikopo ya elimu ya juu, hatua ambayo imewakomboa familia za kipato cha chini na watoto wenye hali duni kuendelea na masomo yao na kujikomboa kutoka katika hali ya umasikini. Pia, tunaipongeza Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kwa kuunda mamlaka ya utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia Zanzibar (ZPRA) na ongezeko la mishahara kwa asilimia 100 kwa wafanyakazi Serikalini.

UWT inatia shime utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi na upanuzi wa viwanja vya ndege, barabara za juu (flyovers), ujenzi wa reli kwa kiwango cha standard gauge, ununuzi wa vivuko, meli na ujenzi wa madaraja makubwa.

Wanawake nchini kote tumepata faraja kubwa kwa hatua ya Serikali kuondoa ushuru, kodi na tozo za kero kwenye mazao na biashara ndogo ndogo, kupanda kwa bei ya mazao ya biashara kama vile Korosho na Pamba kumewakomboa wanawake wakulima vijijini. UWT inaitaka Serikali kuhakikisha Halmashauri zote zinatenga asilimia 10 ya mapato kwa ajili ya wanawake na vijana pamoja na kupeleka milioni 50 kwa kila kijiji ili zitumike kutoa mikopo kwa wajasiriamali na uimarishaji wa benki ya wanawake. Usambazaji wa huduma za maji na umeme vijijini kumeendelea kuondoa uzito mkubwa uliokuwa unawakabili wanawake vijijini wa kutafuta maji kutoka umbali mrefu, pamoja na mafanikio hayo tunaitaka Serikali kuongeza juhudi katika usambazaji wa maji hasa katika maeneo ya vijijini.

UWT inaungana na wanawake wote kuishukuru Serikali kwa kuboresha huduma za Afya na kupunguza vifo vya kina mama wajawazito na watoto chini ya miaka mitano (5), ununuzi wa mashine na vifaa tiba ikiwemo usambazaji wa dawa na vitanda hospitalini, vituo vya afya na zahanati. Kama ilivyotajwa kwenye ilani ya CCM ya 2015/2020, UWT tunasisitiza na kuitaka Serikali kutimiza lengo la kuwa na Zahanati katika kila kijiji, Kituo cha Afya kila Kata na Hospitali kila Wilaya, jambo hili liende sambamba na ujenzi wa maghala ya kisasa ya Bohari ya Dawa (MSD) mikoani.

Aidha, Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT) imeridhishwa na mwelekeo na kasi ya serikali kufikia uchumi wa viwanda, hatua za ujenzi na uzinduzi wa viwanda mbalimbali nchini kote. Mabadiliko ya sera na sheria ya uchimbaji wa madini, mafuta na gesi yanatoa faraja na matumaini makubwa kwa Watanzania hasa wanawake kuelekea uchumi wa kati.

HALI YA AMANI NA USALAMA;
Katika hatua nyingine UWT inaiunga mkono Serikali na vyombo vya ulinzi na usalama kwa hatua mbalimbali wanazochukua kukabiliana na hali ya uvunjifu wa amani na mauaji yanayoendelea katika maeneo mbalimbali nchini kama vile Kibiti, Rufiji na Mkuranga. Unyama uliofanywa hauvumiliki kwani umesababisha wanawake wengi kubaki wajane wakihangaika na ulezi wa watoto na familia zao. Tunatoa wito kwa wanawake, wanasiasa, viongozi wa dini na wananchi kuungana pamoja kukemea na kumuomba Mwenyezi Mungu kutuondolea janga hili. Tunasisitiza Serikali kuongeza nguvu zaidi ili kumaliza kabisa matukio hayo.

Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT) tumesikitishwa sana na tunalaani vikali kauli zilizotolewa na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa zenye viashiria vya kuchochea uvunjifu wa amani na umoja wa kitaifa. Nchi yetu Mwenyezi Mungu ameibariki sana, ni nchi ya umoja, amani, upendo, heshima na mshikamano. Kauli hizo zinazotolewa zinavunja heshima ya viongozi wakuu wa nchi, heshima ya Serikali na Bunge Tukufu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Tunatoa wito kwa wanawake wenzetu na wananchi kutounga mkono, kujitenga na kuzipinga kauli hizo zisizo na staha kwa viongozi, zinazolenga kuleta mfarakano katika jamii yetu.

Aidha, tunatoa msisitizo kwa vyombo vya ulinzi na usalama kuendelea kuchukua hatua kali dhidi ya wale wote wanaotoa kauli zenye viashiria vya wazi vya kuchonganisha Watanzania na kuvuruga amani ya nchi. Serikali iendelee kukemea na kuchukua hatua bila kuhofia hadhi, cheo ama sura ya mtu ili mradi amevunja sheria za nchi.

UWT tunaendelea kuhimiza wanawake na watanzania kufanya kazi kwa bidii, juhudi na maarifa ili kujikomboa na umasikini na kuchangia maendeleo ya nchi. Wanawake na vijana ndio nguvu kazi inayotegemewa kuliendeleza Taifa.

Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) tumepokea kwa furaha kubwa taarifa ya matokeo ya kidato cha sita mwaka 2017, yaliyoonesha watoto wa kike kuongoza kufanya vizuri katika mitihani yao. Tunawapongeza na kuwasisitiza watoto wa kike kuongeza juhudi na kujituma zaidi ili waendelee kufanya vizuri kwani wanao uwezo wa kufanya vizuri zaidi.

UWT tunatoa wito kwa wanawake na wananchi wote, kumuunga mkono Mheshimiwa Rais kwa kujituma na kufanya kazi. Tufanye KILA LINALOWEZEKANA kulinda, kuimarisha Utaifa na Umoja wetu. Tulinde heshima za viongozi wetu na kujiepusha na kauli, matendo na mipango yenye kulenga kudhohofisha Utanzania wetu.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

Imetolewa na:
  
Amina Nassor Makillagi (MNEC, MB)
KATIBU MKUU WA UWT

19/07/2017
Share:

Monday, July 10, 2017

HUDUMA YA MSAADA WA KISHERIA CHINI YA RC MAKONDA WANUFAISHA WAKAZI 80, 000 DAR

NA MWANDISHI MAALUM
Aakiitikia agizo la Rais John Pombe Magufuli alilowataka wateule wake kuwa wabunifu na kujituma ili kuwaondolea wananchi shida mbalimbali , Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, ametatua migogoro takribani 8, 000 iliyowahusisha zaidi ya watu 80, 000 ndani ya takribani miezi minane kati ya Disemba mwaka jana na Mwezi Juni mwaka huu.

Makonda ametekeleza jukumu hilo kupitia timu ya wanasheria 35 wanaojitolea kutoa huduma ya msaada wa kisheria bure kwa wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam.

Kiongozi wa timu ya Wanasheria hao, Georgia Kamina, aliitaja baadhi ya migogoro ambayo timu yake imekuwa ikisuluhisha kupitia Ofisi za Wakuu wa Wilaya zote za mkoa wa Dar es Salaam kuwa ni ile ya umiliki wa ardhi na michakato ya mirathi mahakamani na katika ngazi ya familia,
Migogoro mingine ambayo timu hiyo ya wanasheria imekuwa ikimsaidia Makonda kuitatua kwa kushirikiana na Wakuu wa wilaya ya Ilala  (Sofia Mjema), Kinondoni (Ally Hapi), Temeke (  Felix Lyaniva ), Ubungo (Kisare Makori ) na Kigamboni (_Hashimu Mgandilwa ) ni pamoja na  ndoa na matunzo ya watoto kwa ndoa zilizo sambaratika,  ajira na mikataba ya ajira, ubakaji, faili kupotea mahakamani, ucheleweshwaji wa kesi mahakamani, umiliki wa nyumba,  umiliki au mauziano ya ardhi, mikopo kutoka mabenki ya biashara, uuzwaji mali mbalimbali kwa kukiuka sheria au makubaliano na hata ukosefu wa uaminifu.

Akizungumza kwa niaba ya Makonda, katika Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Ilala Boma, Kamina, alitaja migogoro wanayopokea na  inayotia fora katika mkoa wa Dar es Salaam  kuwa ni ile inayohusisha masuala ya mirathi, umiliki wa ardhi, ajira na mikataba kati ya waajiri na waajiriwa, ndoa na matunzo ya watoto kwa ndoa zilizo sambaratika na baadhi ya wananchi kuingia mikataba mibovu na mabenki katika harakati za kupata mitaji ya biashara.

Sehemu ya Jiji la Dar es Salaam
"Mheshimiwa Paul  Makonda alichukua jukumu la kuanzisha huduma ya msaada wa  kisheria bure kwa wananchi kutokana na uzoefu alioupata katika ziara ya kukutana na wananchi aliyofanya mkoa mzima mwezi Novemba mwaka jana," alibainisha Kamina na kuongeza kuwa ili kuwaepusha wananchi na mchakato mrefu na unaoumiza wa kumaliza migogoro yao mahakamani aliamua kuunda timu ya wanasheria wa kujitolea ili kutekeleza dhamira hiyo ya kuwasaidia wananchi wenye migogoro mbalimbali ya kisheria.

Kiongozi wa timu ya wanasheria hao aliongeza kwa kusema kuwa Mkuu wa Mkoa aliguswa na namna baadhi ya wananchi walivyokuwa wakipoteza mashamba, nyumba, mali na hata kufukuzwa kazi kwa uonevu kwa kukosa uelewa wa sheria.

“Ili kupata suluhisho la matatizo hayo hapo juu na kwakuwa yeye binafsi akiwa msaidizi wa Rais kwa mkoa wa Dar es Salaam basi ndio akaja na wazo la kuanzisha kitengo cha kutatua migogoro ya kisheria kwa njia ya kutoa huduma ya msaada kisheria bila malipo kwa wananchi katika kila wilaya ya mkoa wa Dar es Salaam.

"Tupo jumla ya wanasheria 35 ambao tumegawanyika katika Wilaya zote za mkoa wa Dar es Salaam yaani  Ilala, Kinondoni, Temeke, Ubungo na Kigamboni. Tukiwa katika Ofisi za Wakuu wa Wilaya nilizotaja tunafanya kazi nao kwa karibu sana na pengine wakati mwingine tunajumuika na  Makatibu Tawala  wa Wilaya husika (DAS) na hata wakati mwingine Wakurugenzi Watendaji wa manispaa za mkoa wa Dar es Salaam katika kutatua migogoro hiyo kisheria,” alifichua Mkuu huyo wa Timu ya Wanasheria.

Akizungumzia uzoefu waliopata katika kipindi cha miezi saba walichofanya kazi ya kutoa huduma ya msaada wa kisheria bure  kwa wananchi kwa kusuluhisha migogoro mbalimbali wamegundua wananchi wengi ama hawana au wana uelewa mdogo wa sheria na kila wakati wanafanya makosa makubwa ya kisheria yanayoishia kuwaumiza kimaisha.

"Kuna kina baba na kina mama wengi tu wamekuja mara baada ya kunyang'anywa nyumba zao na mabenki kutokana na kukubali kutoa hati za nyumba hizo kudhamini mikopo ya jamaa zao wakiamini kuwa kama kutakuwa na kutokuelewana kati ya mabenki na ndugu zao nyumba hizo hazitauzwa jambo ambalo sio kweli," alisimulia Kamina.

Akitaja baadhi ya migogoro iliyowagharimu muda na juhudi za ziada kuisuluhisha, Kamina alitaja mgogoro wa umiliki wa ardhi ya hekari 28 unaomhusisha Ogwari Nashon na wakazi wa kijiji cha Viwege, Mbondela eneo la Chanika katika Wilaya ya Ilala.

“Mgogoro huu ulifika mahala ukahatarisha maisha ya ndugu Nashon kwani baadhi ya wanakijiji wasioheshimu sheria walivamia eneo lake, kuchoma moto majengo na kuharibu mazao kama mihogo, mananasi na michungwa.

Mara baada ya Nashon kuja ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Ilala alikutanishwa na wanasheria wa  Mkuu wa Mkoa  wanaotoa huduma ya msaada wa kisheria  bure kwa wananchi walioko wilayani hapo na kueleza tatizo lake ambapo timu yetu iliingilia kati  kwa kushirikiana na Mkuu wa wilaya ya Ilala Sofia Mjema, ili kupata ufumbuzi wa mgogoro huo.

Ni jambo la kutia faraja kwa sasa tumepiga hatua kubwa kuelekea kutatua mivutano iliyokuwepo kwani Nashon ana vielelezo halali vya nyaraka za kiserikali zinazothibitisha umiliki wa eneo hilo," alibainisha Kamina.

Licha ya kujitokeza picha nzuri iliyojaa mafanikio ya huduma hii ya msaada wa kisheria kwa wananchi   katika  Mkoa wa Dar es Salaam, Habari Leo imearifiwa juu ya changamoto lukuki zinazowakabili watoa huduma hiyo katika kutekeleza majukumu yao.
Baadhi ya changamoto hizo ni wananchi kutokuwa na uelewa wa sheria, kanuni na taratibu za kukopa fedha kwa watu binafsi na katika taasisi za fedha, wananchi hawana uelewa wa sheria na taratibu za mirathi na hata wasimamizi wa mirathi hawajui wajibu wao kwa warithi na kwa mahakama jambo ambalo linapelekea warithi kuchelewa au kutopatiwa haki zao hata baada ya mchakato wa mirathi kukamilika katika Mahakama.

“Katika eneo la ajira huko ndio kunatisha kwa uvunjaji wa sheria za ajira na nchi uliokithiri kwani makampuni mengi hasa ya ujenzi na ulinzi hayatoi mikataba ya ajira kwa wafanyakazi, wakati mwingine mikataba inakuja kutolewa baada ya mwajiriwa kuwa amekwisha fanya kazi muda mrefu na inapotolewa inakuwa inakiuka makubaliano ya awali,” alisema na kuwanyooshea kidole viongozi wa serikali za mitaa na kata, katika baadhi ya maeneo kwa kuwa chanzo cha migogoro kwa kufanya majukumu ambayo si yao kisheria na uendeshwaji wa kesi mahakamani kuchukua muda mrefu pasipo na sababu za msingi huku Mabaraza ya kata nayo kuwa dhaifu katika kutekeleza majukumu yake ya kimsingi katika kuwahudumia wananchi na hasa wale wa kipato cha chini.
Akizungumzia huduma hiyo, Makonda alisema aliamua kuanzisha huduma ya msaada wa kisheria kupitia wanasheria hawa (35) katika kila wilaya ya mkoa wa Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya chama tawala Chama Cha Mapinduzi (CCM) inayoagiza kusikiliza na kutatua kero au malalamiko ya wananchi.

Mkuu huyo wa Mkoa alifafanua kuwa katika ziara ya mkoa wa Dar es Salaam mwishoni mwa mwaka 2016 aligundua  wananchi wengi hawakuwa na uelewa wa sheria jambo lililowafanya kupoteza haki zao aidha kwa kutapeliwa, kuonewa au kutojua mahala sahihi pa kupeleka matatizo hayo.

"Pamoja na changamoto nyingi zinazoambatana na huduma hii ya kutafuta suluhu ya matatizo ya wananchi kwa kuzileta pande husika mezani kuongea bado nina dhamira ya kuendelea kuwasaidia Watanzania wenzangu kwa juhudi na maarifa yangu yote.
Na hii ndio gharama ya kuteuliwa na Rais, unapoteuliwa na Mkuu wa nchi anakuwa na matarajio mengi kutoka kwako. Mimi nimeamua kufanya ninayoweza kwa nguvu na juhudi zote ili kumuondolea Rais John Pombe Magufuli na mashinikizo juu ya shida mbalimbali za Wana Dar es Salaam," alimaliza Makonda.
Share:

Monday, July 3, 2017

theNkoromo Blog


Share:

Monday, March 13, 2017

JK AZINDUA TAASISI YAKE YA KUSAIDIA JAMII DUNIANI

 Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete (kulia), akizungumza alipokuwa akizindua rasmi Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF) ikiwa ni sehemu pia ya uzinduzi wa taasisi hiyo kwenye Hotel ya Hyatt Kempinsk The Kilimanjaro Dar es Salaam leo. Kikwete ni Mwenyekiti wa Taasisi hiyo.
 Mwenyekiti wa Taasisi hiyo, Jakaya Kikwete, alisema kuwa Taasisi hiyo pamoja na mambo mengine  itajihusisha na masuala ya Maendeleo ya Binadamu nchini, Afrika na Duniani.
 Kikwete akizungumza na baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Taasisi yake ya JMKF
 Jakaya Kikwete akikumbatiana na Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Taasisi hiyo, Balozi wa zamani wa Marekani nchini Tanzania, Charles Stith
 Mwenyekiti wa Taasisi ya JMKF, Jakaya Kikwete akisalimiana na mjumbe wa Bodi hiyo, Mfanyabiashara maarufu Mtanzania aishie Marekani, Genevieve Sangudi
 Mwenyekiti wa Taasisi ya JMKF, Jakaya Kikwete akisalimiana na mjumbe wa Bodi hiyo ya Wadhamini , Dato' Sri Idris Jala, Waziri asiye na Wizara Maalumu Ofisi ya Waziri Mkuu wa Malaysia na Mtendaji Mkuu wa Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (Pamendu) nchini humo.
 Mwenyekiti wa JMKF, Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la Taasisi hiyo.
 Jakaya akijadiliana jambo na Balozi Charles Stith
 Kikwete akizungumza wakati wa uzinduzi wa Taasisi hiyo.
 Jakaya Kikwete akifafanua mambo mbalimbali kuhusu Taasisi hiyo

 Dato' Sri Idris Jala kutoka Malaysia
 Genevieve Sangudi kutoka Marekani
 Mwanasheria Maarufu nchini, Balozi Mwanaidi  Sinare Maajar. Alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza 2006 na Marekani 2013 Daktari Bingwa wa Upasuasi, Profesa Wiliam Mahalu
 Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa  Rwekaza Mukandara
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kundi la Makampuni la SS Bakhresa, Abubakar Bakhresa
 Balozi wa zamani wa Marekani nchini, Charles Stith
Share:
CCM BLOG. Powered by Blogger.
There was an error in this gadget

Google+ Followers